Upungufu wa madini muhimu Ili nyanya iweze kustawi vizuri katika kila hatua yake ya ukuaji inahitaji virutubisho au madini muhimu, Panapokosekana madini hayo au virutubisho hivyo nyanya huweza kuonyesha dalili mbalimbali za upungufu wa madini husika. Yafuatayo ni madini au virutubisho na dalili zake endapo zitakosekana katika zao la nyanya. 1) Madini ya nitrogen (N) Ni madini muhimu kwa ajili ya ukuaji hasa utengenezaji wa majani ya rangi ya kijani kibichi. Madini haya huitajika sana wiki chache baada ya kupandikiza. Rangi ya kijani ni muhimu kwa nyanya na hata kwa mazao mengine ili mmea uweze kutengeneza chakula chake. Naitrogeni inapokosekana katika mmea rangi ya kijani hupauka na kuwa njano na hatimaye mmea kudumaa. Pia naitrogeni inapotumika kwa wingi kupita kiasi husababisha mmea kuwa na majani mengi bila ya matunda na hivyo kuathiri matunda. Kunapokuwa na upungufu wa naitrogeni inashauriwa kutumia mbolea za chumvi kama CAN, UREA, SA na NPK. 2)Madini ya fosforasi (P) Ni...