Misitu ni mjumuisho wa uoto asilia wenye miti mingi ya aina mbalimbali. Misitu
pia hujumuisha mime ana nyasi zinazoweza kuwa ndefu au fupi.
Aina ya misitu
Misitu asilia
Hii ni aina ya misitu inayoota yenyewe bila kupandwa na mwanadamu. Mfano
Mininga, miombo na mikoko ni aina ya misitu inayoweza kuota yenyewe bila kupandwa.
Misitu ya kupandwa.
Hii ni misitu inayoota baada ya kupandwa na mwanadamu na kwa kiasi Fulani
ukuaji wa misitu hii hutegemea juhudi zitazowekwa. Mfano wa misitu hii ni
milingoti, mipaina na mikaratusi
Tanzania tumejaaliwa kwa kiasi kikubwa kuwa na misitu ya aina zote (Asilia
nay a kupanda). Misitu yetu imekuwa na tija kubwa sana kuhakikisha mifumo ya
kimazingira inakaa saw ana pia watu huajiriwa au kujiajiri kupitia misitu yetu.
Aidha Wanyama na binadamu tunategemea uoto uliopo ili kuendesha Maisha ya
kila siku. Misitu hutupatia madawa ya kujitibu na magonjwa, chakula, matunda,
kuimarisha mfumo wa mzunguko wa mvua (hydrological cycle) na mengine mengi.
Hivyo kutokana na umuhimu mkubwa wa misitu, ni muhimu kuhakikisha misitu
yetu tunailinda, tunaitunza na tunaiimarisha ili iweze kuwa na mchango mkubwa Zaidi
kwetu.
Tukutane katika Makala ijayo tukiwa tunaangazia njia bora za kutunza
misitu yetu.
Comments
Post a Comment