Skip to main content

Posts

Showing posts with the label Nafaka

Mazao ya nafaka

Nafaka ni mbegu za mimea jamii ya nyasi ambazo hutumika kama chakula cha binadamu. Mimea hiyo hutumiwa Zaidi kama chakula cha watu duniani Nafaka hizo ni pamoja na uwele, mtama, mchele, mahindi, ngano, shayiri, ulezi. Japokuwa mazao ya nafaka ni mengi, lakini Mahindi, mchele na ngano ndio mazao yanayolimwa na kuvunwa kwa kiasi kikubwa Zaidi duniani kote. Mazao ya nafaka yanakiasi kikubwa cha wanga (carbohydrate) n ani chanzo muhimu sana cha lishe kwa watu. Vyakula vitokanavyo na mazao ya nafaka ni kama vile ugali, uji, mandazi, chapati, mkate, tambi (spanghett). Kiujumla ni kwanza mazao ya nafaka ni mazao muhimu sana duniani kote kwa sababu ndio chanzo kikubwa cha chakula na hutumiwa na watu wengi. Katika nchi ya Tanzania mikoa ya kusini imekuwa ikifanya vizuri sana katika uzalishaji wa mazao ya nafaka (mazao ya vyakula) na kusaidia kuondoa tatizo la njaa linaloweza tokea endapo chakula hakitoshi. Mazao ya chakula yanaweza kuuzwa na kuchangia katika kuongeza uchumi na mapat...