Utangulizi
Kwa kawaida ni
muhimu kukijua kitu kabla ya kukifanya au kukitumia. Ndugu msomaji karibu upate
kujifunza kuhusu maliasili.
Katika hii dunia,
kila nchi ina maliasili zake japo tunatofautiana kwa uwingi na aina ya
maliasili hizo.
Na Tanzania kama
nchi, tunazo maliasili nyingi sana ambazo zinatusaidia katika Maisha yetu ya
kila siku.
Maliasili ni nini?
Maliasili ni
rasilimali asilia zinazopatikana kwenye nchi husika, kwa upande wetu, ni
rasilimali asilia zote zinazopatikana Tanzania. Rasilimali hizo huweza kuwa
Misitu, mimea, gesi, milima, Wanyama, ardhi na nyinginezo. Tazama Twiga kama
maliasili hapo chini
Kwa maendeleo
endedelevu, ni muhimu sana kuweka juhudi kwenye kuzijua, kuzitunza na
kuziboresha maliasili zetu.
Mfano kutunza vyanzo
vya maji ni muhimu sana kwa sababu maji yanachochea maendeleo katika sekta
karibia zote, hivyo maji yakitunzwa tutapata maendeleo kizazi chetu na kizazi
kijacho.
Aidha utunzaji wa Wanyama
wetu asilia ni muhimu kwa maendeleo yetu kwani itapelekea kukuza pato la taifa
kutokana na utalii lakin pia itaimarisha mtandao wa mzunguko wa chakula na
mazingira.
Kutokana na umuhimu
unaoweza kuzalishwa na maliasili zetu, ni muhimu kwa jamii kujikita katika
kujifunza, kutunza, na kuboresha maliasili
zetu.
Kwa nyongeza, kuzijua maliasili kutakusaidia kufahamu namna nzuri ya kchagua
na kutumia maliasili hizo kwaajili ya shughuli mbalimbali za kiuchumi.
Comments
Post a Comment