Skip to main content

Wajue sangala

Sangara ni Samaki kutoka kwenye familia ya latidae n ani Samaki wa maji baridi. Asili ya Samaki jamii ya sangara ni mto naili na baadhi ya mito kadhaa. Pia Samaki hawa wanapatikana kwa kiasi kidogo katika maji baridi yaliyo changamana na maji chumvi (Brackish water).

Katika nchi za afrika mashariki, sangala amekuwa miongoni mwa Samaki muhimu sana kiuchumi na chakula. Sangara kama Samaki wengine ina kiasi kikubwa sana cha protini na hivyo nilshe muhimu sana.


Sangara ni Samaki anaekula nyama (carnivore) na hvyo anaweza kula Samaki wenzake na kupelekea kupungua kwa hifadhi ya Samaki wengine.

Sangara anao uwezo wa kukua na kufikia urefu wa mita mbili na kuwa na uzito wa kilo 200. Hivyo ni Samaki anaeweza kukua sana Academic

Nchini Tanzania Sangara wanapatikana kwa wingi ziwa viktoria. Katika ziwa viktoria wapo baadhi ya wakulima wanaofuga sangara kwa kutumia vizimba (Pens and Cages).

Hivyo unayo fursa ya kuwekeza katika ufugaji wa sangara katika ziwa viktoria na kukuza uchumi. Samaki hawa hupendwa zaid sehemu mbalimbali za duniani


Comments

Popular posts from this blog

Kambale ni nani?

Kambale ni samaki wenye umbo la mkunga na wenye sharubu (whisker) katika vichwa vyao. Kambale wanapatikana nchi za Afrika na mashariki ya kati. Kambale wanaishi kwenye maji baridi ya mito, maziwa, mikondo ya maji na mabwawa. Pia kambale huweza kuishi kwenye matope au maeneo yenye maji kidogo. Kambale walianza kufugwa miaka ya 1970 katika maeneo mbalimbali ya ulimwengu kama ilivyoainishwa na  Wikipedia .    Kwa kawaida kambale wanaweza kukua mpaka kufikia urefu wa mita 1.7 na kufikia uzito wa kilo 60 kama ilivyoelezwa na  Froose . Kambale wanakula nyama pamoja na mboji. Na kutokana na ukubwa wa mdomo wa kambale, kambale anaweza kumeza nyama kubwa kiasi. Sifa za kambale Kambale hukua haraka na huweza vyakula vya aina nyingi Kambale ni wagumu na huvumilia mazingira magumu Kambale wanaweza kufugwa wengi kwa pamoja  Kambale hawazaliani kwenye mabwawa ya kufugia bali hukua tuu Kambale huweza kukaa nje ya maji kwa muda mrefu zaidi kutokana na uwe

Wajue sato

Sato ni samaki wa mwanzo kufugwa tangu miaka 3000 iliyopitta kama inavyoelezwa huko misri. Na mpaka sasa Sato ni miongoni mwa samaki anaefugwa kwa kiasi kikubwa nchi za Africa na duniani kiujumla. Sato ni samaki wanaoweza kuishi kwenye maji baridi. Samaki hawa hupatikana kwenye mito, mikondo ya maji baridi, mabawawa au maziwa na mara chache hupatikana sehemu zenye mchanganyiko wa maji chumvi na maji baridi (Brackish water) Hivyo kutokana na mazingira ambayo sato wanaweza kuishi, unayo fursa ya kuweza kufuga sato kwenye maji baridi. Mfano, unaweza kufuga samaki hawa kwenye mito, maziwa au mabwawa ya kuchimba na ya kujenga. Sato huzaliana kwa kutaga mayai. Kwa mzunguko mmoja sato mmoja ana uwezo wa kutaga mayai kuanzia 1500-2000. Na kwa kawaida sato hutaga mayai kwa mizunguko minne mpaka nane kwa mwaka. Sato pia wana uwezo mkubwa wa kuvumilia kiasi kidogo cha hewa ya oksijeni (Oxygen). Na kwa upande wa chakula, sato wana uwezo wa kula vyakula mbalimbali (Wana uwanda mpana wa vyakula).  W