Skip to main content

Kilimo cha nyanya

 Utangulizi

Zao la nyanya ni zao ambalo hulimwa dunia nzima.Kwa Tanzania zao la nyanya hutumika katika matumizi ya kila siku ya chakula.Nyanya ni miongoni mwa zao la mboga mboga inayopatikana katika jamii ya solanaceae,mazao mengine maarufu yanayopatikana katika jamii hii ni pilipili hoho,bilinganya,nyanya chungu na viazi mviringo.Pia zao la nyanya limeonekana kutengeneza pesa nyingi kuliko mazao mengine yalioko katika jamii hiyo ya solanaceae hivyo huweza kuinua uchumi wa mkulima.Pia zao la nyanya linahitaji umakini mkubwa katika matumizi ya pembe jeo.

 

 

  Hali ya hewa

Nyanya hustawi vizur katika hali ya hewa yenye nyuzi joto Kati ya 21-32C.Kiwango cha maji ambacho kinahitajika ni 1880mm kwa msimu mzima.Kwa maana hiyo nyanya huweza kustawi katika maeneo ya joto kuliko katika maeneo ya baridi.

     Udongo

Nyanya hukua vizuri katika udongo tifutifu wenye rutuba ambao hautuamishi maji,pia huweza kustawi katika udongo mfinyanzi na kichanga.kiasi cha pH ya udongo inayohitajika katika zao la nyanya ni Kati ya 5.5-7.5.ili kuyajua yote hayo ni vizuri kuwatafuta wataalam wa utafiti wa udongo kwa sababu udongo huweza hata kuhifadhi magonjwa.

     Aina za nyanya

Kuna aina kuu mbili za nyanya ambazo ni.

1) Nyanya zinazokua ndefu(indeterminate)

Aina hii ya nyanya hukua na kuzaa kwa mda mrefu husogekwa kwa kutumia miti mirefu,kamba ndefu na wakati mwingine nyaya hutumika.Nyanya aina hii hupendeza zaidi katika kilimo cha ndani(greenhouse).Mkulima anaweza kulima aina hii ya nyanya nje lakini anahitajika kuwa na nguvu kazi kubwa kwa ajili ya kuekea miti.Ukilima ndani unaweza kuvuna nyanya hii kwa mida wa miezi tisa mfululizo na ukilima nje unaweza kuvuna miezi sita mfululizo.Mfano wa mbegu hii ni Anna F1,uwezo,Eva F1 n.k.Hivyo kuuliza mtaalamu ili uweze kujua aina ya nyanya ni jambo muhimu.



2) Nyanya fupi/determinate

Hizi ni nyanya zina zokua na kikomo cha kujua kwa mda mfupi .huvunwa kwa muda mfupi kiasi cha miezi 2-4.Ni nyanya zinazoshauriwa kulimwa kibiashara na wakulima wenye mashamba makubwa ,aina hii ya  nyanya huwekewa miti mifupi.Mfano wa aina hii ya mbegu ni Tanya,mwanga n.k

Pia katika hizo aina mbili za mbegu kuna mbeg ni vizuri  chotara/hybrid na mbegu za kuboreshwa ,ila mbegu chotara hushauriwa zaidi kutumika.

Mfano wa mbegu chotara ni Ann kwasababu husaidia a F1,Kile F1,Kipato F1,Milele F1 n.k.

Na mfano wa mbegu zilizoboreshwa ni Tengeru 97, Tanya n.k.

 

    Mahitaji ya mbegu

Ni muhimu kutumia mbegu bora kila wakati . kiasi cha gramu 50-100 ya mbegu hutosha kupanda hekari moja kutegemeana na njia ya usiaji, uotaji na nafasi ya kupanda. Mbegu ya nyanya huota baada ya siku 4-8.

        Kusia vitaru

kuna aina mbili ya vitaru, Vitaru sinia(tray) na vitaru vya chini. Vitaru sinia ni vizuri sana kwani husaidia kuepuka magonjwa ya ardhini pia husadia miche kukua kwa haraka zaidi.

Vitaru vya chini pia vimegawanyika kuna vitaru mbinuko na vitaru mbonyeo. Vitaru mbinuko ni vizuri 

kwa sababu husaidia hewa kuzunguka kwa urahisi.

Kwa kawaida miche ya nyanya huwa tayari kwa kupandwa shambani baada ya siku 21 tangia kusia mbegu.

 

 lookaside.fbsbx.com/lookaside/crawler/media/?media...          

 

 

        Maandalizi ya shamba

Lima shamba(matuta) kwa kina ch 30-45 na kisha andaa matuta yenye upana wa sentimita 150 kutoka katikati ya tuta moja na jingine.Umuhimu wa kutumia matuta huweza kusambaza vyema mizizi na kupata virutubisho, Unyevu na hewa. Matuta pia huondoa maji mengi yaliyojaa shambani.

        Upandaji

Nyanya hupandwa kwa umbali wa nafasi ya sentimita 30 mche na mche na sentimita 60 mstari kwa mstari hii ni kwa mbegu za kawaida. Kwa mbegu chotara inashauriwa mche na mche iwe sentimita 60 na mstari na mstari iwe sentimita 90.

Panda kwa kutumia mbolea kianzio(starter solution), Hii unaweza kuitengeneza mwenyewe kwa kutumia DAP. Chukua 3kg za DAP na weka kwenye maji lita 200, hakikisha wakati unaweka hiyo mbolea kianzia hayo maji yasiguse majanj ya miche.





 KATIKA MAKALA YAJAYO TUTAANGALIA NAMNA YA KUWEKA MITI NA HUDUMA NYINGINE ZA SHAMBA KAMA VILE UEKAJI WA MBOLEA N.K


         Uwekaji wa miti

Nyanya ni mimea yenye shina laini lisiloweza kusimama wima bila usaidizi, Hivyo iko kuweza kuongeza uzalishaji kwa kuepuka magonjwa ni muhimu mimea ya nyanya iweze kuwekewa miti ili isimame imara bila kutambaa ardhini. Zipo aina nyingi za uekaji wa miti kutegemeana na aina ya nyanya , Kama ni fupi au ndefu na pia hutegemea na upatikanaji wa vifaa kama vile miti/fito,waya, N.k

Uwekaji miti hupunguza mashambulizi ya magonjwa na wadudu kwa kuruhusu mzunguko wa hewa kupitia vema na kuongeza ukuaji mzuri kwa kuruhusu mwanga kupenya kwa urahisi. Kwa ekari muja inahitaji miti 1800 urefu ni mita 1.5-2 kamba mita 15000 ambayo itakuwezesha kufunga mizunguko mitatu weka mita kwa muda muafaka kabla ya kupanda au baada ya kupanda na isizidi siku 14 na mti na mti weka 150cm usipungue hapo watu wengi hukosea huweka 200cm au 300cm na mimea ina anguka kwa hiyo maana ya kufunga kamba inakua haipo.

     Kupunguza machipukizi/Maotea.

Ni muhimu kwa nyanya ndefu kuondoa machipukizi na kubakia shina moja au mawili tu ili kupunguza msongamano na hivyo mimea huzaa matunda yenye ubora wa kutosha. Kwa nyanya fupi hakuna sababu ya kupunguzia lakini majani hupunguza matunda yanapokaribia kukomaa.


       Palizi.

Magugu hushindana na mazao katika kugombea virutubisho, mwanga, hewa na unyevu. Magugu ni moja ya visumbufu kwa mazao. Shamba lililojaa magugu huvutia wadudu na vimelea vya magonjwa kuweza kujifucha na kufanya mashambulizi kwa mazao hivyo sharti udhibiti wa magugu shambani, kama palizi, kung'oa kwa mkono, kutumia viuagugu kabla na baada ya kupanda, kabla ya kupanda kama shamba Lina majani unashauriwa kutumia viuagugu vinavyoua magugu yote mfano wa viuagugu hivo ni;

          1)Kalach 480 SL(glyphosate 360g/e) 

         2)Volsate 360 SL( Glyphosate 360).

    Viuagugu hivyo vitumike kabla hujapanda, Viuagugu vifuatavyo vinaweza kutumika baada ya kupanda kwa sababu haviwezi kuathiri mimea hiyo.

           1)Pantera 40 EC (Quizalofop-P-Tefuryl 40)

         2)Centurion 120 EC (Clethodim 120 g/e)

    Viuagugu hivyo huua magugu aina ya nyasi tu, kama kuna magugu/ majani yenye majani mapana hayatakufa na hivyo unashauriwa kukagua shamba lako kuangalia aina ya magugu na kama ni nyasi ndio utumie hivi viuagugu tofauti na hapo usitumie.

         Mbolea/Fertilizer.

    Nyanya kama yalivyo mazao mengine huhutaji rutuba ya kutosha yenye virutubisho mbalimbali kama vile naitrojeni, fosfirasi, potasiam, manganizi, kalsiamu n.k. Virutubisho hivyo vinahitajika kwa kiwango na wakati tofauti tofauti na hufanywa kazi tofauti kwa mmea, kwa hiyo ni muhimu kuweka mbolea zenye virutubisho vyote kwa wakati muafaka ili kupata mazao bora.

    Unapopanda nyanya anza na starter iliyotengenezwa kutoka kwenye DAP, kutengeneza hiyo starter changanya 3kg ya DAP kwenye maji Lita 200 na kisha weka 250ml kwa kila shina, hakikisha maji ya mbolea hiyo hayagusi majani.

    Baada ya siku 5-7 na weka DAP au yara otesha au NPK, kiasi cha 5g kwa kila shina na baada ya siku 21 tangia uweke DAP kiasi cha 5g kwa kila shina, baada ya siku 14-21 weka CAN kiasi cha 5-10g kwa kila shina.Baada ya kueka mbolea hizi subiri siku 21 na weka MOP kiasi cha 5-10g kwa kila shina na endelea na kuweka CAN, NPK na MOP kwa kubadili kila baada ya siku 21 hadi mwisho wa mavuno.

       KATIKA MAKALA IJAYO TUTAELEZEA UPUNGUFU WA MADINI KATIKA ZAO LA NYANYA.


    Comments

    Popular posts from this blog

    Wajue sangala

    Sangara ni Samaki kutoka kwenye familia ya latidae n ani Samaki wa maji baridi. Asili ya Samaki jamii ya sangara ni mto naili na baadhi ya mito kadhaa. Pia Samaki hawa wanapatikana kwa kiasi kidogo katika maji baridi yaliyo changamana na maji chumvi (Brackish water). Katika nchi za afrika mashariki, sangala amekuwa miongoni mwa Samaki muhimu sana kiuchumi na chakula. Sangara kama Samaki wengine ina kiasi kikubwa sana cha protini na hivyo nilshe muhimu sana. Sangara ni Samaki anaekula nyama (carnivore) na hvyo anaweza kula Samaki wenzake na kupelekea kupungua kwa hifadhi ya Samaki wengine. Sangara anao uwezo wa kukua na kufikia urefu wa mita mbili na kuwa na uzito wa kilo 200. Hivyo ni Samaki anaeweza kukua sana  Academic Nchini Tanzania Sangara wanapatikana kwa wingi ziwa viktoria. Katika ziwa viktoria wapo baadhi ya wakulima wanaofuga sangara kwa kutumia vizimba (Pens and Cages). Hivyo unayo fursa ya kuwekeza katika ufugaji wa sangara katika ziwa viktoria na kukuza uchumi. S

    Kambale ni nani?

    Kambale ni samaki wenye umbo la mkunga na wenye sharubu (whisker) katika vichwa vyao. Kambale wanapatikana nchi za Afrika na mashariki ya kati. Kambale wanaishi kwenye maji baridi ya mito, maziwa, mikondo ya maji na mabwawa. Pia kambale huweza kuishi kwenye matope au maeneo yenye maji kidogo. Kambale walianza kufugwa miaka ya 1970 katika maeneo mbalimbali ya ulimwengu kama ilivyoainishwa na  Wikipedia .    Kwa kawaida kambale wanaweza kukua mpaka kufikia urefu wa mita 1.7 na kufikia uzito wa kilo 60 kama ilivyoelezwa na  Froose . Kambale wanakula nyama pamoja na mboji. Na kutokana na ukubwa wa mdomo wa kambale, kambale anaweza kumeza nyama kubwa kiasi. Sifa za kambale Kambale hukua haraka na huweza vyakula vya aina nyingi Kambale ni wagumu na huvumilia mazingira magumu Kambale wanaweza kufugwa wengi kwa pamoja  Kambale hawazaliani kwenye mabwawa ya kufugia bali hukua tuu Kambale huweza kukaa nje ya maji kwa muda mrefu zaidi kutokana na uwe

    Wajue sato

    Sato ni samaki wa mwanzo kufugwa tangu miaka 3000 iliyopitta kama inavyoelezwa huko misri. Na mpaka sasa Sato ni miongoni mwa samaki anaefugwa kwa kiasi kikubwa nchi za Africa na duniani kiujumla. Sato ni samaki wanaoweza kuishi kwenye maji baridi. Samaki hawa hupatikana kwenye mito, mikondo ya maji baridi, mabawawa au maziwa na mara chache hupatikana sehemu zenye mchanganyiko wa maji chumvi na maji baridi (Brackish water) Hivyo kutokana na mazingira ambayo sato wanaweza kuishi, unayo fursa ya kuweza kufuga sato kwenye maji baridi. Mfano, unaweza kufuga samaki hawa kwenye mito, maziwa au mabwawa ya kuchimba na ya kujenga. Sato huzaliana kwa kutaga mayai. Kwa mzunguko mmoja sato mmoja ana uwezo wa kutaga mayai kuanzia 1500-2000. Na kwa kawaida sato hutaga mayai kwa mizunguko minne mpaka nane kwa mwaka. Sato pia wana uwezo mkubwa wa kuvumilia kiasi kidogo cha hewa ya oksijeni (Oxygen). Na kwa upande wa chakula, sato wana uwezo wa kula vyakula mbalimbali (Wana uwanda mpana wa vyakula).  W