Skip to main content

Posts

Showing posts with the label Kambale

Kambale ni nani?

Kambale ni samaki wenye umbo la mkunga na wenye sharubu (whisker) katika vichwa vyao. Kambale wanapatikana nchi za Afrika na mashariki ya kati. Kambale wanaishi kwenye maji baridi ya mito, maziwa, mikondo ya maji na mabwawa. Pia kambale huweza kuishi kwenye matope au maeneo yenye maji kidogo. Kambale walianza kufugwa miaka ya 1970 katika maeneo mbalimbali ya ulimwengu kama ilivyoainishwa na  Wikipedia .    Kwa kawaida kambale wanaweza kukua mpaka kufikia urefu wa mita 1.7 na kufikia uzito wa kilo 60 kama ilivyoelezwa na  Froose . Kambale wanakula nyama pamoja na mboji. Na kutokana na ukubwa wa mdomo wa kambale, kambale anaweza kumeza nyama kubwa kiasi. Sifa za kambale Kambale hukua haraka na huweza vyakula vya aina nyingi Kambale ni wagumu na huvumilia mazingira magumu Kambale wanaweza kufugwa wengi kwa pamoja  Kambale hawazaliani kwenye mabwawa ya kufugia bali hukua tuu Kambale huweza kukaa nje ya maji kwa muda mre...