Skip to main content

Posts

Showing posts with the label Mbogamboga&Matunda

kilimo cha nyanya

 Upungufu wa madini muhimu  Ili nyanya iweze kustawi vizuri katika kila hatua yake ya ukuaji inahitaji virutubisho au madini muhimu, Panapokosekana madini hayo au virutubisho hivyo nyanya huweza kuonyesha dalili mbalimbali za upungufu wa madini husika. Yafuatayo ni madini au virutubisho na dalili zake endapo zitakosekana katika zao la nyanya. 1) Madini ya nitrogen (N) Ni madini muhimu kwa ajili ya ukuaji hasa utengenezaji wa majani ya rangi ya kijani kibichi. Madini haya huitajika sana wiki chache baada ya kupandikiza. Rangi ya kijani ni muhimu kwa nyanya na hata kwa mazao mengine ili mmea uweze kutengeneza chakula chake. Naitrogeni inapokosekana katika mmea rangi ya kijani hupauka na kuwa njano na hatimaye mmea kudumaa. Pia naitrogeni inapotumika kwa wingi kupita kiasi husababisha mmea kuwa na majani mengi bila ya matunda na hivyo kuathiri matunda. Kunapokuwa na upungufu wa naitrogeni inashauriwa kutumia mbolea za chumvi kama CAN, UREA, SA na NPK. 2)Madini ya fosforasi (P) Ni...

Kilimo cha nyanya

 Magonjwa ya nyanya 1)Bakajani wahi ( Early blight) Ni ugonjwa wa fangasi ni ukungu unaoshambulia mimea ya nyanya kwa kiasi kikubwa. Ugonjwa huu hushambulia zaidi katika kipindi cha mvua. Dalili za ugonjwa huu ni kua na madoa madogo madogo yenye rangi nyeusi au rangi ya kahawia kwenye majani hasa ya chini, matunda na shina. Miche midogo kwenye kitalu inaposhambuliwa hunyauka na kufa, na Miche mikubwa hudondosha majani na matunda na kunyauka kwa shina na hatimaye kufa. Udhibiti Hakikisha Usafi wa shamba na ng'oa masalia ya mazao na kuchoma moto mara moja baada ya kuvuna. Pia zingatia mzunguko wa mazao na pia tumia mbegu ambazo hupinga ugonjwa huu(Resistant varieties) . Viuatilifu ambavyo vinaweza kutumika ni kama vile EVITO T 477 SC, GLORY 750 WG (MANCOZEB), CUPROCAFFARO 50 WP (COPPER OXYCHLORIDE) 2)Bakajani chelewa (Late blight) Ni ugonjwa  hatari sana haswa kipindi cha mvua na baridi ya wastani. Dalili za ugonjwa huu ni kuwa na mabaka makubwa yenye majimaji kwenye matunda, Sh...

Kilimo cha nyanya

 Utangulizi Zao la nyanya ni zao ambalo hulimwa dunia nzima.Kwa Tanzania zao la nyanya hutumika katika matumizi ya kila siku ya chakula.Nyanya ni miongoni mwa zao la mboga mboga inayopatikana katika jamii ya solanaceae,mazao mengine maarufu yanayopatikana katika jamii hii ni pilipili hoho,bilinganya,nyanya chungu na viazi mviringo.Pia zao la nyanya limeonekana kutengeneza pesa nyingi kuliko mazao mengine yalioko katika jamii hiyo ya solanaceae hivyo huweza kuinua uchumi wa mkulima.Pia zao la nyanya linahitaji umakini mkubwa katika matumizi ya pembe jeo.       Hali ya hewa Nyanya hustawi vizur katika hali ya hewa yenye nyuzi joto Kati ya 21-32C.Kiwango cha maji ambacho kinahitajika ni 1880mm kwa msimu mzima.Kwa maana hiyo nyanya huweza kustawi katika maeneo ya joto kuliko katika maeneo ya baridi.      Udongo Nyanya hukua vizuri katika udongo tifutifu wenye rutuba ambao hautuamishi maji,pia huweza kustawi katika udongo mfinyanzi na kichanga.kiasi cha pH ...

Mimea yetu ya matunda

Hii ni mimea inayotupatia matunda na mazao mbalimbali. Mazao ya matunda pia huweza kuwa ya asili au ya kupandwa. Mfano wa mimea asilia ya matunda ni mifenesi inayopatikana porini. Mfano wa mimea ya matunda ni miembe, mipera, michikichi, minazi, michungwa, milimao, parachichi, ndizi, michenza, mbuni, zabibu na hiliki. Mimea ya matunda inaweza kuzalisha mazao mengine kama vile Dawa, Mafuta, Juisi au viungo vya chakula. Mazao ya matunda ni chakula pendwa kwa watu mbalimbali duniani. Ulaji wa matunda unaenda sambamba sana na uimarikaji wa afya na hupunguza matatizo mengi sana ya afya. Mazao ya matunda pia ni chanzo muhimu sana cha mapato na uchumi endapo matunda yatauzwa ndani au nje ya nchi. Tanzania imejaaliwa matunda mengi sana, hivyo ni muhimu kuwekeza katika kilimo cha matunda kwa maendeleo endelevu. Makala ijayo itaangazia Mahitaji muhimu ya kilimo cha matunda.