Hii ni mimea inayotupatia matunda na mazao mbalimbali. Mazao ya matunda pia huweza kuwa ya asili au ya kupandwa. Mfano wa mimea asilia ya matunda ni mifenesi inayopatikana porini. Mfano wa mimea ya matunda ni miembe, mipera, michikichi, minazi, michungwa, milimao, parachichi, ndizi, michenza, mbuni, zabibu na hiliki. Mimea ya matunda inaweza kuzalisha mazao mengine kama vile Dawa, Mafuta, Juisi au viungo vya chakula. Mazao ya matunda ni chakula pendwa kwa watu mbalimbali duniani. Ulaji wa matunda unaenda sambamba sana na uimarikaji wa afya na hupunguza matatizo mengi sana ya afya. Mazao ya matunda pia ni chanzo muhimu sana cha mapato na uchumi endapo matunda yatauzwa ndani au nje ya nchi. Tanzania imejaaliwa matunda mengi sana, hivyo ni muhimu kuwekeza katika kilimo cha matunda kwa maendeleo endelevu. Makala ijayo itaangazia Mahitaji muhimu ya kilimo cha matunda.