Utangulizi Kwa kawaida ni muhimu kukijua kitu kabla ya kukifanya au kukitumia. Ndugu msomaji karibu upate kujifunza kuhusu maliasili. Katika hii dunia, kila nchi ina maliasili zake japo tunatofautiana kwa uwingi na aina ya maliasili hizo. Na Tanzania kama nchi, tunazo maliasili nyingi sana ambazo zinatusaidia katika Maisha yetu ya kila siku. Maliasili ni nini? Maliasili ni rasilimali asilia zinazopatikana kwenye nchi husika, kwa upande wetu, ni rasilimali asilia zote zinazopatikana Tanzania. Rasilimali hizo huweza kuwa Misitu, mimea, gesi, milima, Wanyama, ardhi na nyinginezo. Tazama Twiga kama maliasili hapo chini Kwa maendeleo endedelevu, ni muhimu sana kuweka juhudi kwenye kuzijua, kuzitunza na kuziboresha maliasili zetu. Mfano kutunza vyanzo vya maji ni muhimu sana kwa sababu maji yanachochea maendeleo katika sekta karibia zote, hivyo maji yakitunzwa tutapata maendeleo kizazi chetu na kizazi kijacho. Aidha utunzaji wa Wanyama wetu asilia ni muhimu kwa maendeleo yetu k...