Magonjwa ya nyanya
1)Bakajani wahi ( Early blight)
Ni ugonjwa wa fangasi ni ukungu unaoshambulia mimea ya nyanya kwa kiasi kikubwa. Ugonjwa huu hushambulia zaidi katika kipindi cha mvua.
Dalili za ugonjwa huu ni kua na madoa madogo madogo yenye rangi nyeusi au rangi ya kahawia kwenye majani hasa ya chini, matunda na shina. Miche midogo kwenye kitalu inaposhambuliwa hunyauka na kufa, na Miche mikubwa hudondosha majani na matunda na kunyauka kwa shina na hatimaye kufa.
Udhibiti
Hakikisha Usafi wa shamba na ng'oa masalia ya mazao na kuchoma moto mara moja baada ya kuvuna. Pia zingatia mzunguko wa mazao na pia tumia mbegu ambazo hupinga ugonjwa huu(Resistant varieties) .
Viuatilifu ambavyo vinaweza kutumika ni kama vile EVITO T 477 SC, GLORY 750 WG (MANCOZEB), CUPROCAFFARO 50 WP (COPPER OXYCHLORIDE)
2)Bakajani chelewa (Late blight)
Ni ugonjwa hatari sana haswa kipindi cha mvua na baridi ya wastani.
Dalili za ugonjwa huu ni kuwa na mabaka makubwa yenye majimaji kwenye matunda, Shina na hata majani.
Mabaka yenye majimaji hutokea hasa sehemu ya juu ya matunda. Mimea inaposhambuliwa na ugonjwa huu hufa katika kipindi kifupi.
Udhibiti
Zingatia kilimo cha mzunguko wa mazao, hakikisha unapalilia vizuri, tumia matandazo na ondoa masalia ya mazao shambani mara baada ya kuvuna.
Viuatilifu vinavyoweza kutumika kudhibiti ugonjwa huu ni kama vifuatavyo BANKO 500 SC, CUPROCAFFARO 50 WP, EVITO na GLORY 750 WG ( MANCOZEB)
3)Madoadoa na mnyauko bacteria ( bacterial wilt)
Ugonjwa huu husababishwa na bacteria ambao husababisha mnyauko na kufa kwa mmea ghafla.
Dalili za ugonjwa huu huonekana mara tu matunda yanapoanza, Bacteria wanaosababisha ugonjwa huu huishi ardhini katika udongo kwa mda mrefu na hushambulia mimea kupitia mizizi, Au majeraha katika mimea wakati wa kuhamisha Miche kutoka kitaluni na kupandikiza, Mazingira ambayo bacteria hawa hupendelea ni hali ya joto na unyevu katika udongo.
Vimelea hawa wakishaingia katika mishipa ya mimea huziba njia za mfumo wa mzunguko wa maji katika mimea hivyo mimea hunyauka kwa haraka Bali rangi ya kijani hubakia na bila madoa. Dalili hii husaidia kutofautiaha na mnyauko fusari( fusarium wilt). Dalili nyingine ya ugonjwa huu ni kua mimea huanza kunyauka kutokea juu
Udhibiti
Tumia nyanya zinazo stahimili mashambulizi, tumia mzunguko wa mazao wa muda mrefu, usipande nyanya katika shamba lililopandwa migomba msimu uliopita.
Dawa yenye copper hufanya vizuri katika kupunguza tatizo hili ni kama vile CUPROCAFFARO 50 WP (copper oxychloride).
4)Mnyauko fusari ( fusarium wilt)
Ni ugonjwa hatari wa ukungu/ fangasi.
Dalili za ugonjwa huu kudumaa, kubadilika rangi na kuwa njano na kahawia na kisha kunyauka. Vimelea wa ugonjwa huu huishi ardhini na hushambulia mimea kupitia mizizi, vimelea hawa hushambulia kwa kuziba mishipa ya kupashia maji na hivyo mimea kusinyaa kwa kukosa maji na hatimaye kufa. Mashambulizi ya mnyauko fusari huenda haraka kuliko magonjwa mengine ya mnyauko. Vimelea wa ugonjwa huu huahamiri zaidi katika mazingira yenye udongo wenye majimaji.
Mmea huanza kunyauka kutokea chini kwenda juu.
Udhibiti
Hakuna kiuatilifu kinachotibu ugonjwa huu kwa asilimia mia hivyo inashauriwa baada ya ugonjwa huu kujitikeza ng'oa na choma moto mimea yote iliyoathirika kisha pulizia mimea iliyobaki dawa ya ukungu.
Pia inashauriwa kutumia mzunguko wa mazao ambayo sio jamii ya nyanya.
Pia ni muhimu kudhibiti Minyoo fundo kwani hii hudhoofisha mimea na kurahisisha kupenya kwa mnyauko fusari.
Viuatilifu vifuatavyo vinaweza kupunguza athari kwa asilimia flani ni EVITO T 477 SC na GLORY 750 WG
5)Ugonjwa wa kata kiuno ( Damping off)
Ni ugonjwa unaosababushwa na vimelea vya fangasi. Kewepo kwa msongamano wa mimea na kukosekana kwa mtiririko bora wa maji ardhini hupelekea kuenea kwa ugonjwa huu.
Ugonjwa huu hushambulia zaidi Miche vitaluni.
Dalili za ugonjwa huu ni kunyauka ghafla kwa Miche sentimita chache kutoka ardhini. Maji yakizid ugonjwa huu huathiri zaidi.
Udhibiti
Tumia mbegu ambazo zina chanjo ya mbegu na ni vyema kabla ya kusia kuweka dawa. Chanjo ambayo ni nzuri ni SEED PLUS 30 WS kipimo ni 10g kwenye kila kilo 4 za mbegu.
Pia mara baada ya Miche kuota tumia dawa ya ukungu kama vile IVORY M 72 WP, EVITO T 477 SC na GLORY 750 WG.
Ni muhimu kufuata maelekezo ya wataalamu juu ya utumiaji wa dawa hizo.
6)Ubwiri unga ( powdery mildew)
Huu pia ni ugonjwa wa ukungu dalili zake utaona ungaunga kwenye majani na rangi ya majivu.
Udhibiti
Tumia viuatilifu kama vile EVITO T 477 SC,
EMINENT STAR 312.5 SE na PROCURE 480 SC.
7) Magonjwa ya virusi
Magonjwa haya huambukizwa kupitia mbegu au kusambazwa na wadudu kama inzi mweupe, wadudu mafuta, binadamu na hata vifaa vya kazi.
Mashambulizi makali huonekana wakati wa joto kali na ukame.
Dalili za magonjwa haya ni kudumaa na majani kukunjamana yakipinda kuelekea juu, kutoa matawi mengi na majani kuwa na rangi ya njano, nyeupe au zambarau.
Moja ya magonjwa ya virusi ni TOMATO MOSAIC VIRUS (TMV).
Udhibiti
Ondoa mara moja mimea iliyoahambuliwa na choma moto mbali na shmaba, zingatia Usafi wa shamba, dhibiti wadudu waenezao virus hasa inzi weupe.
MATATIZO MENGINE
MATUNDA KUPASUKA
Matunda huweza kupasuka yanapokua makubwa kukaribua na muda wa kukomaa , Ipo mipasuko ya mviringo na mingine yenye sura ya nyota.
Mipasuko hii hutokana na kutokua na mpangilio mzuri wa umwagiliaji wa maji.
Hali hii hutokea zaidi wakati wa vipindi vya jua kali na mvua vinapofuatana.
Very interesting,I'm now aware of the problems related to tomato production.
ReplyDeleteImprove by providing as much details as possible.