Habari mpenzi msomaji wa Makala zetu. Leo tutaangazia mazao ya biashara yanayoingiza pato kubwa hapa nchini Tanzania. Ndugu msomaji tambua kuwa kuyajua mazao haya ya biashara yanayoingiza pato kubwa, itakusaidia kuchagua zao maalum katika uwanda wa kilimo na biashara. Kitabu cha hali ya uchumi wa taifa (2018) na ofisi ya taifa ya takwimu (NBS) inaeleza kuwa tumbaku, kahawa, chai, korosho na pamba , ni mazao ya biashara yanayoingiza pesa nyingi sana za kigeni. Tumbaku Tumbaku ni zao la biashara linalolimwa mikoa ya Ruvuma, Tabora, Mbeya, Morogoro na Iringa . Kwa mwaka 2018, zao la tumbaku liliongoza kuingiza fedha nyingi Zaidi za kigeni. Tofauti na 2018 zao hili limekuwa likiingiza pesa nyingi kwa wakulima na kukuza pato la taifa. 2. Korosho Mikoa maarufu katika uzalishaji wa korosho ni Mtwara, Lindi, Pwani, Tanga na Ruvuma . Mara nyingi korosho imekuwa ikishika nafasi ya pili katika mazao yanayo ingiza mapato kwa watanzania na serikali kiujumla. ...