Skip to main content

Posts

Kambale ni nani?

Kambale ni samaki wenye umbo la mkunga na wenye sharubu (whisker) katika vichwa vyao. Kambale wanapatikana nchi za Afrika na mashariki ya kati. Kambale wanaishi kwenye maji baridi ya mito, maziwa, mikondo ya maji na mabwawa. Pia kambale huweza kuishi kwenye matope au maeneo yenye maji kidogo. Kambale walianza kufugwa miaka ya 1970 katika maeneo mbalimbali ya ulimwengu kama ilivyoainishwa na  Wikipedia .    Kwa kawaida kambale wanaweza kukua mpaka kufikia urefu wa mita 1.7 na kufikia uzito wa kilo 60 kama ilivyoelezwa na  Froose . Kambale wanakula nyama pamoja na mboji. Na kutokana na ukubwa wa mdomo wa kambale, kambale anaweza kumeza nyama kubwa kiasi. Sifa za kambale Kambale hukua haraka na huweza vyakula vya aina nyingi Kambale ni wagumu na huvumilia mazingira magumu Kambale wanaweza kufugwa wengi kwa pamoja  Kambale hawazaliani kwenye mabwawa ya kufugia bali hukua tuu Kambale huweza kukaa nje ya maji kwa muda mre...

Wajue sato

Sato ni samaki wa mwanzo kufugwa tangu miaka 3000 iliyopitta kama inavyoelezwa huko misri. Na mpaka sasa Sato ni miongoni mwa samaki anaefugwa kwa kiasi kikubwa nchi za Africa na duniani kiujumla. Sato ni samaki wanaoweza kuishi kwenye maji baridi. Samaki hawa hupatikana kwenye mito, mikondo ya maji baridi, mabawawa au maziwa na mara chache hupatikana sehemu zenye mchanganyiko wa maji chumvi na maji baridi (Brackish water) Hivyo kutokana na mazingira ambayo sato wanaweza kuishi, unayo fursa ya kuweza kufuga sato kwenye maji baridi. Mfano, unaweza kufuga samaki hawa kwenye mito, maziwa au mabwawa ya kuchimba na ya kujenga. Sato huzaliana kwa kutaga mayai. Kwa mzunguko mmoja sato mmoja ana uwezo wa kutaga mayai kuanzia 1500-2000. Na kwa kawaida sato hutaga mayai kwa mizunguko minne mpaka nane kwa mwaka. Sato pia wana uwezo mkubwa wa kuvumilia kiasi kidogo cha hewa ya oksijeni (Oxygen). Na kwa upande wa chakula, sato wana uwezo wa kula vyakula mbalimbali (Wana uwanda mpana wa vyakula)....

Mimea yetu ya matunda

Hii ni mimea inayotupatia matunda na mazao mbalimbali. Mazao ya matunda pia huweza kuwa ya asili au ya kupandwa. Mfano wa mimea asilia ya matunda ni mifenesi inayopatikana porini. Mfano wa mimea ya matunda ni miembe, mipera, michikichi, minazi, michungwa, milimao, parachichi, ndizi, michenza, mbuni, zabibu na hiliki. Mimea ya matunda inaweza kuzalisha mazao mengine kama vile Dawa, Mafuta, Juisi au viungo vya chakula. Mazao ya matunda ni chakula pendwa kwa watu mbalimbali duniani. Ulaji wa matunda unaenda sambamba sana na uimarikaji wa afya na hupunguza matatizo mengi sana ya afya. Mazao ya matunda pia ni chanzo muhimu sana cha mapato na uchumi endapo matunda yatauzwa ndani au nje ya nchi. Tanzania imejaaliwa matunda mengi sana, hivyo ni muhimu kuwekeza katika kilimo cha matunda kwa maendeleo endelevu. Makala ijayo itaangazia Mahitaji muhimu ya kilimo cha matunda.  

Sayansi ya udongo

 Coming soon

Mazao ya nafaka

Nafaka ni mbegu za mimea jamii ya nyasi ambazo hutumika kama chakula cha binadamu. Mimea hiyo hutumiwa Zaidi kama chakula cha watu duniani Nafaka hizo ni pamoja na uwele, mtama, mchele, mahindi, ngano, shayiri, ulezi. Japokuwa mazao ya nafaka ni mengi, lakini Mahindi, mchele na ngano ndio mazao yanayolimwa na kuvunwa kwa kiasi kikubwa Zaidi duniani kote. Mazao ya nafaka yanakiasi kikubwa cha wanga (carbohydrate) n ani chanzo muhimu sana cha lishe kwa watu. Vyakula vitokanavyo na mazao ya nafaka ni kama vile ugali, uji, mandazi, chapati, mkate, tambi (spanghett). Kiujumla ni kwanza mazao ya nafaka ni mazao muhimu sana duniani kote kwa sababu ndio chanzo kikubwa cha chakula na hutumiwa na watu wengi. Katika nchi ya Tanzania mikoa ya kusini imekuwa ikifanya vizuri sana katika uzalishaji wa mazao ya nafaka (mazao ya vyakula) na kusaidia kuondoa tatizo la njaa linaloweza tokea endapo chakula hakitoshi. Mazao ya chakula yanaweza kuuzwa na kuchangia katika kuongeza uchumi na mapat...

Mazao ya biashara yanayoingiza pato kubwa Tanzania

Habari mpenzi msomaji wa Makala zetu. Leo tutaangazia mazao ya biashara yanayoingiza pato kubwa hapa nchini Tanzania. Ndugu msomaji tambua kuwa kuyajua mazao haya ya biashara yanayoingiza pato kubwa, itakusaidia kuchagua zao maalum katika uwanda wa kilimo na biashara. Kitabu cha hali ya uchumi wa taifa (2018) na ofisi ya taifa ya takwimu (NBS) inaeleza kuwa tumbaku, kahawa, chai, korosho na pamba , ni mazao ya biashara yanayoingiza pesa nyingi sana za kigeni.   Tumbaku Tumbaku ni zao la biashara linalolimwa mikoa ya Ruvuma, Tabora, Mbeya, Morogoro na Iringa . Kwa mwaka 2018, zao la tumbaku liliongoza kuingiza fedha nyingi Zaidi za kigeni. Tofauti na 2018 zao hili limekuwa likiingiza pesa nyingi kwa wakulima na kukuza pato la taifa.      2. Korosho Mikoa maarufu katika uzalishaji wa korosho ni Mtwara, Lindi, Pwani, Tanga na Ruvuma . Mara nyingi korosho imekuwa ikishika nafasi ya pili katika mazao yanayo ingiza mapato kwa watanzania na serikali kiujumla. ...

Kondoo

 Coming soon