Nafaka ni mbegu za mimea jamii ya nyasi ambazo hutumika kama chakula cha binadamu. Mimea hiyo hutumiwa Zaidi kama chakula cha watu duniani
Nafaka hizo
ni pamoja na uwele, mtama, mchele, mahindi, ngano, shayiri, ulezi.
Japokuwa
mazao ya nafaka ni mengi, lakini Mahindi, mchele na ngano ndio mazao yanayolimwa
na kuvunwa kwa kiasi kikubwa Zaidi duniani kote.
Mazao ya
nafaka yanakiasi kikubwa cha wanga (carbohydrate) n ani chanzo muhimu sana cha
lishe kwa watu.
Vyakula
vitokanavyo na mazao ya nafaka ni kama vile ugali, uji, mandazi, chapati,
mkate, tambi (spanghett).
Kiujumla ni
kwanza mazao ya nafaka ni mazao muhimu sana duniani kote kwa sababu ndio chanzo
kikubwa cha chakula na hutumiwa na watu wengi.
Katika nchi
ya Tanzania mikoa ya kusini imekuwa ikifanya vizuri sana katika uzalishaji wa
mazao ya nafaka (mazao ya vyakula) na kusaidia kuondoa tatizo la njaa linaloweza
tokea endapo chakula hakitoshi.
Mazao ya chakula
yanaweza kuuzwa na kuchangia katika kuongeza uchumi na mapato.
Hivyo unayo
fursa ya kuanzisha kilimo cha mazao ya nafaka na kuingia kwenye biashara ya
mazao hayo.
Comments
Post a Comment