Sato ni samaki wa mwanzo kufugwa tangu miaka 3000 iliyopitta kama inavyoelezwa huko misri. Na mpaka sasa Sato ni miongoni mwa samaki anaefugwa kwa kiasi kikubwa nchi za Africa na duniani kiujumla.
Sato ni samaki wanaoweza kuishi kwenye maji baridi. Samaki hawa hupatikana kwenye mito, mikondo ya maji baridi, mabawawa au maziwa na mara chache hupatikana sehemu zenye mchanganyiko wa maji chumvi na maji baridi (Brackish water)
Hivyo kutokana na mazingira ambayo sato wanaweza kuishi, unayo fursa ya kuweza kufuga sato kwenye maji baridi. Mfano, unaweza kufuga samaki hawa kwenye mito, maziwa au mabwawa ya kuchimba na ya kujenga.
Sato huzaliana kwa kutaga mayai. Kwa mzunguko mmoja sato mmoja ana uwezo wa kutaga mayai kuanzia 1500-2000. Na kwa kawaida sato hutaga mayai kwa mizunguko minne mpaka nane kwa mwaka.
Sato pia wana uwezo mkubwa wa kuvumilia kiasi kidogo cha hewa ya oksijeni (Oxygen). Na kwa upande wa chakula, sato wana uwezo wa kula vyakula mbalimbali (Wana uwanda mpana wa vyakula).
Watu wengi duniani hutumia sato kama chakula na hivyo kupelekea sato kuwa na soko la uhakika.
Hivyo kutokana na sifa mbali mbali za sato, unaweza kufuga sato katika mazingira tofauti tofauti na kupata mazao ya kutosha.
Comments
Post a Comment