Kambale
ni samaki wenye umbo la mkunga na wenye sharubu (whisker) katika vichwa vyao.
Kambale wanapatikana nchi za Afrika na mashariki ya kati.
Kambale
wanaishi kwenye maji baridi ya mito, maziwa, mikondo ya maji na mabwawa. Pia
kambale huweza kuishi kwenye matope au maeneo yenye maji kidogo.
Kambale
walianza kufugwa miaka ya 1970 katika maeneo mbalimbali ya ulimwengu kama
ilivyoainishwa na Wikipedia.
Kwa kawaida kambale wanaweza kukua mpaka kufikia urefu wa mita 1.7 na kufikia uzito wa kilo 60 kama ilivyoelezwa na Froose.
Kambale wanakula nyama pamoja na mboji. Na kutokana na ukubwa wa mdomo wa kambale, kambale anaweza kumeza nyama kubwa kiasi.
Sifa za kambale
- Kambale
hukua haraka na huweza vyakula vya aina nyingi
- Kambale
ni wagumu na huvumilia mazingira magumu
- Kambale
wanaweza kufugwa wengi kwa pamoja
- Kambale
hawazaliani kwenye mabwawa ya kufugia bali hukua tuu
- Kambale
huweza kukaa nje ya maji kwa muda mrefu zaidi kutokana na uwezo wake wa
kutumia hewa ya kawaida isiyo ya maji
Kutokana
na sifa mbalimbali za kambale, ufugaji wa samaki wa jamii ya kambale huweza
kuwa mwepesi zaidi kutokana na uwezo wa kambale kuvumilia mazingira magumu ya
ufugaji
Mimi ni mfugaji wa kambale na nimefika muda wa mavuno nahitaji wateja 0762504270
ReplyDelete