Habari mpenzi msomaji wa Makala zetu. Leo tutaangazia mazao ya biashara yanayoingiza pato kubwa hapa nchini Tanzania.
Ndugu msomaji
tambua kuwa kuyajua mazao haya ya biashara yanayoingiza pato kubwa, itakusaidia
kuchagua zao maalum katika uwanda wa kilimo na biashara.
Kitabu cha hali ya
uchumi wa taifa (2018) na ofisi ya taifa ya takwimu (NBS) inaeleza kuwa tumbaku,
kahawa, chai, korosho na pamba, ni
mazao ya biashara yanayoingiza pesa nyingi sana za kigeni.
- Tumbaku
Tumbaku ni zao la biashara linalolimwa mikoa ya Ruvuma, Tabora, Mbeya, Morogoro na Iringa. Kwa mwaka 2018, zao la tumbaku liliongoza kuingiza fedha nyingi Zaidi za kigeni. Tofauti na 2018 zao hili limekuwa likiingiza pesa nyingi kwa wakulima na kukuza pato la taifa.
2. Korosho
Mikoa maarufu katika uzalishaji wa korosho ni Mtwara, Lindi, Pwani, Tanga na Ruvuma. Mara nyingi korosho imekuwa ikishika nafasi ya pili katika mazao yanayo ingiza mapato kwa watanzania na serikali kiujumla.
3. Kahawa
Kahawa imekuwa ni zao
la kibiashara linalotegemewa Zaidi mikoa ya Kagera,
Ruvuma, Mbeya, Kilimanjaro, Kigoma, Arusha na Mara. Zao la kahawa huingiza mapato makubwa kwa wananchi
na serikali kiujumla na hivyo kukuza GDP.
4. Pamba
Zao la pamba limekuwa
likilimwa sana mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Mwanza na Singida. Mauzo ya zao hili yamekuwa yakiwanufaisha sana
wananchi na kukuza uchumi wao.
5. 5. Kahawa
Mbeya, Arusha, Tanga, Iringa na Njombe ni baadhi ya mikoa inayojikita katika kilimo cha zao
la chai. Kwa mwaka 2018, zao la chai lilishika nafasi ya 5 kwa mazao yanayoingiza
pato kubwa hapa Tanzania.
Makala zijazo tutachambua kila zao na namna unavyoweza kuanzisha kilimo cha mazao hayo na kuyafanyia biashara kwa ufanisi
Comments
Post a Comment