Sangara ni Samaki kutoka kwenye familia ya latidae n ani Samaki wa maji baridi. Asili ya Samaki jamii ya sangara ni mto naili na baadhi ya mito kadhaa. Pia Samaki hawa wanapatikana kwa kiasi kidogo katika maji baridi yaliyo changamana na maji chumvi (Brackish water). Katika nchi za afrika mashariki, sangala amekuwa miongoni mwa Samaki muhimu sana kiuchumi na chakula. Sangara kama Samaki wengine ina kiasi kikubwa sana cha protini na hivyo nilshe muhimu sana. Sangara ni Samaki anaekula nyama (carnivore) na hvyo anaweza kula Samaki wenzake na kupelekea kupungua kwa hifadhi ya Samaki wengine. Sangara anao uwezo wa kukua na kufikia urefu wa mita mbili na kuwa na uzito wa kilo 200. Hivyo ni Samaki anaeweza kukua sana Academic Nchini Tanzania Sangara wanapatikana kwa wingi ziwa viktoria. Katika ziwa viktoria wapo baadhi ya wakulima wanaofuga sangara kwa kutumia vizimba (Pens and Cages). Hivyo unayo fursa ya kuwekeza katika ufugaji wa sangara katika ziwa viktoria na kukuza uchumi. S
Comments
Post a Comment