Skip to main content

Mifugo kwa maendeleo endelevu

Mbuzi ni mnyama anaepatikana kwenye familia ya Bovidae chini yake Caprinae. Kuna Zaidi ya jamii 300 za mbuzi. Kutokana na Ushahidi wa akiolojia (archaeology), mbuzi ni Wanyama wa mwanzo kuanza kufugwa kwa Zaidi ya miaka 10,000 iliyopita Sciences


Mazao yatokanayo na mbuzi ni kama maziwa, ng’ombe, Ngozi, nyam ana mbolea. Pia kutokana na maziwa ya mbuzi tunaweza kupata Jibini (Cheese)

Mbuzi wanao uwezo wa kuishi katika mazingira magumu, yakiwemo mazingira yenye ukame. Pia mbuzi wanaweza kuvumilia magonjwa kutokana na miili yao kuwa na kinga nzuri.

Mbuzi wana tabia ya kula kwa kuvinjari vichaka (browsing).

Katika mazingira ya Tanzania, Unaweza kufuga mbuzi takribani maeneo yote ya Tanzania bila kupata changamoto kubwa.

Gharama za uendeshaji wa ufugaji wa mbuzi ni ndogo n ahata mtaji wa kuanzia kufugia ni mdogo.

Hivyo unayo fursa ya kuwekeza katika ufugaji wa mbuzi na kupata mazao mbalimbali yatokanayo na mbuzi.

Karibu katika Makala zijazo tuzochambua mfumo mzima wa ufugaji wa mbuzi.


Comments